Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa dunia lazima wawekeze katika takwimu bora kuhusu watoto

Viongozi wa dunia lazima wawekeze katika takwimu bora kuhusu watoto

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEFlinatoa wito wa viongozi wa dunia kuwekeza katika takwimu bora kuhusu watoto. Bryan Lenhander na maelezo zaidi.

(TAARIFA YA BRYAN)

Shirika hilo limeonya katika tathimini mpya kwamba takwimu zilizopo sasa ninusua ya viashiria vya malengo ya maendeleo endelevu kuhusu watoto.

Tathimini ya UNICEF inaonyesha kwamba takwimu zinazohusiana na watoto za masuala kama ya umasikini na ukatili ambazo zinaweza kulinganishwa ama ni chache mno au hazina ubora , hivyo kuziacha serikali bila taarifa inazohitaji ili kuweza kushughulikia changamoto zinazowakabili mamilioni ya watoto, lakini pia kuwa vigumu kufuatilia hatua zilizopigwa katika mchakato wa kufikia malengo ya maendeleo endelevu.

Twakimu zingine zinazokosekama ni za ukatili wa kingono, vifo vya watoto wakati wa kujifungua kudumaa na uzito wa kupindukia kwa watoto.