Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utafiti wabaini simu ya kiganjani yaokoa wakimbizi wengi

Utafiti wabaini simu ya kiganjani yaokoa wakimbizi wengi

Kuelekea mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu wakimbizi na wahamiaji hapo wiki ijayo, Shirika la umoja huo la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema simu ya kiganjani yasalia mwokozi kwa wakimbizi wengi. Rosemary Musumba na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Rosemary)

Video hiyo ikiwa na sauti za waigizaji mashuhuri akiwemo Cate Blachet, balozi mwema wa UNHCR, yaeleza vitu muhimu ambavyo wakimbizi huvibeba pindi masaibu yanapowapata… chakula, maji, mahema… lakini simu ya kiganjani ndio zaidi..

Utafiti wa UNHCR na kampuni ya Accenture umebaini kuwa mawasiliano ya simu za kiganjani au rununu pamoja intaneti ni muhimu sana kwa usalama wao na kwa ajili ya kurahisha mawasiliano wao na jamii zao.

Wakimbizi wengi wanapatia umuhimu sana kuwa na simu hiyo ili wapate habari zinazowahusu ikiwemo pia huduma za jamii.

Utafiti huo ulifanywa katika nchi 44 katika mabara manne ambapo Kamishna Mkuu wa UNHCR Filippo Grandi amesema kuwa katika dunia ya sasa simu ya kiganjani na intaneti ni usalama kwa wakimbizi.