Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usugu wa tiba ya magonjwa ya zinaa waibua mwongozo mpya

Usugu wa tiba ya magonjwa ya zinaa waibua mwongozo mpya

Shirika la Afya Duniani, WHO leo limezindua mwongozo mpya wa matibabu ya magonjwa ya zinaa ambayo ni pangusa, kisonono na kaswende. Taarifa zaidi na Brian Lehander.

(Taarifa ya Brian)

WHO imechukua hatua hiyo kutokana na ongezeko la usugu wa magonjwa hayo kwa dawa za antibayotiki zinazotumika hivi sasa.

Magonjwa hayo yanasababishwa na bakteria na hutibika lakini WHO inasema mara nyingi kubainika kwake huchukua muda na watu hutumia vibaya dawa na hivyo kuleta usugu.

Takwimu zinaonyesha kuwa kila mwaka zaidi ya watu milioni 131 huugua pangusa, milioni 78 kisonono na zaidi ya milioni tano na nusu huugua kaswende. Nathalie Broutet ni mtaalam kutoka WHO anasoma magonjwa hayo yasipotibiwa vyema husababisha madhara ya kiafya ikiwemo ujauzito kutoka na ugumba na utasa, hivyo .

(Sauti Natalie)

“Tunataka kuhakisha kwamba nchi zinapata mikakati sahihi ya matibabu, ili nchi hizi ziweze kusahihisha matibabu yao ya kitaifa na kuzitumia kwa kutumia mikakati hii”