Hali Darayya ni mbaya- de Mistura
Nchini Syria, hali halisi katika jimbo la Daraya ni hatari na ya kutisha amesema mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria, Staffan de Mistura. Taarifa zaidi na Amina Hassan.
(Taarifa ya Amina)
Katika taarifa yake, de Mistura amesema tangu mwezi Novemba mwaka 2012 kumekuwepo na wito wa kuondoa kuzingirwa kwa eneo hilo, lakini halisikilizwi, halikadhalika wito wa kusitisha mapigano.
Mjumbe huyo ameongeza kuwa amejulishwa kuhusu makubaliano yaliyofikiwa usiku ya kuhamisha raia na wapiganji kuanzia leo jambo ambalo amesema Umoja wa mataifa haukuhusishwa na pande zote mbili.
Hata hivyo amesema ni muhimu sana kulinda wakazi wa Darayya katika operesheni hiyo na kwamba mchakato huo ufanyike kwa hiyari.
Bw.Bw. Staffan de Mistura anamsiihi mwenyekiti mwenza wa maswala ya kuleta amani Syria pamoja na wajumbe wa patanishi kulitilia msisitizo swala la utekelezaji wa mkataba huu na matokeo katika viwango vya umoja wa mataifa.