Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kabumbu na utangamano baina ya wakimbizi na wenyeji DRC

Kabumbu na utangamano baina ya wakimbizi na wenyeji DRC

Huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC wakimbizi wanaendelea kumiminika kutoka nchi jirani zinazokumbwana madhila ikiwemo Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR. Wakimbizi hao licha ya maisha ya magumu wanaendeleza vipaji vyao vya shughuli wanazopenda ikiwemo michezo. Miongoni mwao ni mkimbizi kutoka CAR ambaye yeye ni msakata kabumbu na anaamini michezo ni mbinu si tu ya kuburudisha bali pia kuleta utangamano kama anavyosimulia Flora Nducha kwenye makala hii.