Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanariadha wakimbizi wa Sudan Kusini wanaelekea Brazil leo

Wanariadha wakimbizi wa Sudan Kusini wanaelekea Brazil leo

Wanariadha watano wakimbizi wa Sudan Kusni ambao hadi hivi karibuni walikuwa kambini Kakuma Kenya, leo wameendoka Nairobi kuelekea Brazil tayari kwa michuano ya Olimpiki.

Wanariadha hao wamesindikizwa kwa mbembwe, shangwe na nderemo , na marafiki zao, wakimbizi wenzao na raia wa Kenya, vyote hivyo vikighubikwa na machozi ya furaha, kuagana na nyimbo za kuwatia moyo, kwani mbali ya kuwalisha wakimbizi ni tukio la kihistoria.

Wakimbizi hao wanawake wawili na wanaume watatu watakwenda kuungana na wenzao watano kutoka Syria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na Ethiopia , ili kuandika historia ya kushiriki katika timu ya kwanza kabisa ya wakimbizi katika michuano ya olimpiki. Michuano hiyo ya kimataifa ya olimpiki inaanza rasmi Agost 5.