Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada watakiwa kati ya mmiminiko wa wakimbizi wa Sudan Kusini, UNHCR

Msaada watakiwa kati ya mmiminiko wa wakimbizi wa Sudan Kusini, UNHCR

Msaada zaidi utahitajika kukidhi mahitaji ya wakimbizi wa Sudan Kusini wanaotazamiwa kuzidi milioni moja, ikiwa mgogoro utaendelea kuwalazimisha kukimbia makwao, amesema, Ann Encontre, Mratibu wa kikanda wa wakimbizi wa Sudan Kusini. John Kibego na taarifa kamili

(Taarifa ya John Kibego)

Akiongea kwenye uzinduzi wa wito wa dola milioni 701 jijini Nairobi, Kenya hii leo, Bwana Encontre alionyenya hofy ya uwezekano watu zaidi kukimbia mzozo wa kijeshi mjini Juba na kusababisha uhaba wa ufadhili kwa wakimbizi wa Sudan Kusini.

Amesema, kwa sasa wamepokea asilimia kumi na saba ya mchango wa dola milioni 638 walizosaka kutoka mwanzo kwa ajili ya mwaka huu.

Bwana Encontre, amesema hiki kimewalazimisha kutoa kipaumbele kwa uitikio wa dharura na harakati za kuokoa maisha, badala ya mahitaji muhimu kama maji, vifaa vya kujisafi, afya na malazi kwa wakimbizi hao.