Skip to main content

Ujumbe muafaka kwa amani kupitia sanaa ya mwimbaji Tania Kassis

Ujumbe muafaka kwa amani kupitia sanaa ya mwimbaji Tania Kassis

Juhudi za kuedeleza amani duniani huchukua sura na nyenzo tofauti katika Umoja wa Mataifa. Moja ya nyenzo hizo ni sanaa. Katika juhudi zake hizo, na kwa kushirikiana na msanni Tania Kassis kutoka Lebanon, Umoja huo umetoa wimbo ambao unaonyesha dhahiri madhila wanayokumbana nayo watu kote ulimwenguni, hususan kule ambako kunashuhudiwa mizozo.

Mwimbaji huyo ameimba wimbo wenye ujumbe mzito katika lugha tatu. Basi ungana na Grace Kaneiya katika makala hii, inayojumuisha pia wimbo huo kwa jina, Al Ardou Lil Jami3