Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkakati wa kukomesha ukatili dhidi ya watoto wazinduliwa

Mkakati wa kukomesha ukatili dhidi ya watoto wazinduliwa

Mkakati wa kimataifa kukomesha ukatili dhidi ya watoto umezinduliwa na wataalamu wa afya wa Umoja wa mataifa hii leo.

Likizindua mpango huo Shirika la afya duniani WHO limesema , mtazamo huo wa kimataifa unahitajika kwani nyanyasaji kuathiri watoto bilioni moja kila mwaka.

WHO inasema licha ya takwimu za kutisha, visa vingi vya unyanyasaji vinafichwa, havionekani au haviripotiwi. Ulinzi wa watoto dhidi ya unyanyasaji upo chini ya sheria za kimataifa , na hasa ndani ya mkataba wa haki za mtoto (CRC)

Licha h ya hayo utafitio wa karibuni wa WHO unaonyesha kwamba hadi watoto bilioni moja wamekabiliwa na unyanyasaji kwa mwaka 2015, ukiwa ni pamoja na wa kimiwli, kingono au kisaikolijia. Na hii ni sawa na mtoto mmoja kila watoto wawili. Dr Alex Butchart wa WHO anasema tatizo ni kubwa lakini halitiliwi maanani.

(SAUTI YA DR ALEX)

Tunazungumzia aina za unyanyasaji ambao unaathiri watoto mara nyingi katika nchi zote , na huu ni unyanyasaji binafsi, sio vita, sio unyanyasaji wa pamoja, lakini unyanyasaji wa ana kwa ana”

Kati ya watoto wote wanaoathirika , mmoja kati ya wanne ni mhanga wa unyanyasaji wa kimiwli, na mmoja kati ya wasichana watano amepitia unyanyasaji wa kingono.

Na utafiti unasema katika baadhi ya nchi mauaji pia ni moja ya sababu zinazoongoza za vifo kwa barubaru. Dr Alex amesema ili kuweza kufikia malengo ya maendeleo endelevu ni lazima kukomesha unyanyasi dhidi ya watoto.

Na kufanikisha hilo miradi mbalimbali inaanzishwa kusaidia watoto akitolea mfano miradi iliyofanikiwa kama ile ya malezi nchini Kenya, Liberia na Myanmar. Wakati nchi kama Zambia mradi wa ushauri nasaha umesaidia saana kuponya watoto walioathirika na unyanyasaji, kisaikolojia.