Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kennedy Lawford ateuliwa kuwa balozi mwema wa UNODC

Kennedy Lawford ateuliwa kuwa balozi mwema wa UNODC

Balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na madawa ya kulevya na uhalifu UNODC Christopher Kennedy Lawford anasema kuwa amehitimu kwa njia ya kipekee kuchukua wadhifa huo.

Kennedy Lawford ambaye ni mpwa wa rais wa zamani wa Marekani John F. Kennedy pia ni mcheza filamu na pia ameishi kama mtawaliwa wa madawa ya kulevya ya heroin. Bwana Kennedy ambaye pia amehitimu shahada ya uanasheria anasema kuwa anafahamu jinsi ya kuzungumza na watawaliwa wa madawa ya kulevya, waunda sera ,wanasiasa na hata mawaziri.

Kennedy aliteuliwa kuchukua wadhifa huo na mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayopambana na madawa ya kulevya na uhalifu Yuri Fedotov.