Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kimataifa wa nyuklia kukabili tisho la ugaidi wafanyika Wanshington

Mkutano wa kimataifa wa nyuklia kukabili tisho la ugaidi wafanyika Wanshington

Wawakilishi kutoka karibu nchi 50 wanakutana mjini Washington leo kwa ajili ya mkutano wa usalama wa nyuklia ulioandaliwa na Rais wa Marekani Barack Obama.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anahudhuria mkutano huo kwani anaona usalama wa nyuklia kama moja ya tishio kubwa linaloikabili dunia kwa sasa. Ban Ki-moon anaenda Washington siku chache tuu baada ya Marekani na Urusi kutia saini makubaliano ya kihistoria ya kupunguza silaha za nyuklia.Na mwezi ujao wa May Ban atakuwa mwenyeji wa mkutano wa kutathimini pande zilizoridhia makubaliano hayo ya kupunguza silaha za nyuklia.

Ban amesema kwa kutiwa saini makubaliano mapya ya START na mkutano ujao wa tathmini basi itaonekana kasi ya kutimiza lengo la kuwa na dunia iliyo huru bila silaha za nyuklia. Lakini kasi hiyo inatishiwa na dhana ya ugaidi wa nyuklia ambayo bwana Ban amesema ni moja ya matishio makubwa kabisa katika dunia ya leo.