Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukabidhi wa jengo la KICC ni ishara ya mkutano wa UNCTAD14 kufanyika

Ukabidhi wa jengo la KICC ni ishara ya mkutano wa UNCTAD14 kufanyika

Kuelekea mkutano wa 14 wa kamati ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo na biashara, UNCTAD, mjini Nairobi, Kenya, hii leo serikali ya Kenya imekabidhi jengo la kimataifa la mikutano la Kenyatta, KICC kuashiria kuwa sasa liko chini ya Umoja wa Mataifa hadi mkutano utakapokamilika tarehe 22 Julai mwaka huu. Mkutano utaanza rasmi tarehe 17 ukitanguliwa na mikutano ya awali kama vile vijana na mashirika ya kiraia. Shuhuda wetu alikuwa Assumpta Massoi na hii hapa ni taarifa yake.

(Taarifa ya Assumpta)

Nje ya jengo la mikutano la kimataifa la Kenyatta, KICC jijini Nairobi, Kenya, shughuli maalum siku ya Jumanne asubuhi ni makabidhiano ya jengo hilo kwa Umoja wa Mataifa. Waziri wa Utalii Najib Balala alikabidhi ufunguo kama ishara kwa waziri wa mambo ya kigeni, Balozi Amina Mohammed ambaye naye hatimaye alikabidhi ufunguo kwa Katibu Mkuu wa UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi. Nilimuuliza Dkt. Kituyi tukio la leo linaashiria nini?

(Sauti dkt. Kituyi)

Na Balozi Amina hakuficha hisia zake.

(Sauti Balozi Amina)