Skip to main content

UNAIDS yazindua ripoti kuhusu kinga dhidi ya Ukimwi

UNAIDS yazindua ripoti kuhusu kinga dhidi ya Ukimwi

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuighulika na masuala ya ukimwi UNAIDS limezindua ripoti mpya kuhusu pengo lililopo katika kinga dhidi ya ukimwi.

Ikiwa na mapendekezo kuhusu namna ya kusitisha maambukizo mapya na kufikia malengo ya 2020 kama ilivyoelezwa kwenye tamko la kisiasa la mwaka 2016 lililofikiwa mjini New York mwezi Juni, ripoti hiyo imetolewa siku chache kabla ya mkutano wa kimataifa kuhusu Ukimwi utakaofanyika mjini Durban nchini Afrika Kusini kaunzia Julai 18 hadi 22 mwaka huu.

Michel Sidibé, ni mkurugenzi mkuu wa UNAIDS anaeleza namna hali ya kinga ilivyo barani Afrika.

( SAUTI MICHEL)

‘‘Ripoti inaonyesha asilani kuwa kinga dhidi ya Ukimwi haifanyi kazi kwa wasichana ukanda wa kusini mwa jangwa la Sahara. Wanahitaji kinga . Kati ya asilimia 75 ya maambukizi mapya barani Afrika, asilimia 10 hadi 19 ni wasichana vigori.’’