Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatoa wito wa kufungua mipaka kwa ajili ya wakimbizi wa Sudan Kusini

UNHCR yatoa wito wa kufungua mipaka kwa ajili ya wakimbizi wa Sudan Kusini

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limetoa wito kwa pande zote hasimu kwenye vita vya Sudan Kusini kuhakikisha watu wanaokimbia vita wanaondoka kwa usalama.

Limeziomba pia nchi jirani kuacha mipaka yake wazi ili kuruhusu wakimbizi wanaosaka hifadhi.

Nalo Shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA likisema watu 36,000 wametawanywa na machafuko hayo na wakimbizi wa ndani 7000 wamechukua hifadhi kwenye kituo cha Umoja wa mataifa.

Leo Dobbs ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA LEO DOBBS)

"Mjini Juba tunasikitishwa na hali ya wakimbizi 9000 kufuatia ripoti za hofu kuhusu hali ya usalama, aidha ugumu wa kupata mahitaji muhimu kama chakula na maji. Maeneo mengine ya kuhifahdi wakimbizi yanaripotiwa kuwa na hali ya utulivu. Kwenye maeneo ya mipaka kumekuwa na tofauti kwa mfano mpakani na Uganda hali ya usalama imeimarishwa nchini Sudan Kusini na hivyo kupelekea idadi ya wakimbizi kutoka Sudan Kusini wanaoelekea nchini Uganda kupungua."