Skip to main content

Duru ya pili ya mazungumzo ya Burundi yaanza

Duru ya pili ya mazungumzo ya Burundi yaanza

Mwenyekiti wa Kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na amani Burundi Balozi Jurg Lauber amekuwa ziarani nchini humo, huku duru ya pili ya mazungumzo ya amani kuanza leo mjini Arusha Tanzania. Ramadhani Kibuga na taarifa kamili

(TAARIFA YA KIBUGA)

Mwenyekiti wa Kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na amani Burundi amekuwa ziarani nchini humo. Jurg Lauber amesititizia umuhimu wa kuinua uchumi wa Burundi kama sehemu pia ya kustaawisha nchi hii. Baada ya mazungumzo yake na Rais wa Bdi Pierre NKURUNZIZA, Balozi huyo wa Uswizi kwenye Umoja wa Mataifa anayefuatilia Burundi alisema waliyojadili

"Tumezungumzia kuhusu umuhumu mkubwa wa sekta ya uchumi hasa ukuaji wa uchumu nchini Burundi,juhudi za amani lakini pia changamoto Bdi inazokumbana nazo. Tumezungumzia pia njia za ushirikiano, nini tume hii ya Umoja wa Mataifa inachoweza kufanya ili kuimarisha uhusianao wa kiuchumi.Tumezungumzia pia uwiano kati ya sekta ya uchumi pamoja na amani na usalama na hasa mazungumzo ya kisiasa."

Naye rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amekaribusha ziara hii na kusema kuwa serikaly yake iko tayari kwa mazungumzo.

Ziara hii imefanyika wakati imeanzishwa hii leo mjini Arusha Tz raundi ya pili ya mazungumzo ya amani kati ya wadau mbalimbali wa siasa za Burundi. Mazungumzo hayo yananuwia kumaliza mgogoro wa kisiasa uliodumu kwa zaidi ya mwaka mzima kutokana na uamzi wa Rais NKUR wa kuwania muhula wa tatu.

Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya watu 500 wameuwawa na raia laki 2 na Elfu 70 kuomba hifadhi katika nchi jirani.

Mimi ni Ramadhani Kibuga, Redio ya Umoja wa Mataifa, Bujumbura.