Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miji Afrika ikiboreshwa vijana hawatakimbilia Ulaya

Miji Afrika ikiboreshwa vijana hawatakimbilia Ulaya

Kongamano la usalama wa miji barani Afrika limezinduliwa mjini Durban nchini Afrika Kusini, shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-Habitat kwa kushirikiana na manispaa ya mji wa Durban wakiwezesha mjadala kuhusu kuboresha miji barani Afrika.

Taarifa kamili na Joshua Mmali.

( TAARIFA YA JOSHUA)

Akiongea wakati wa hafla hiyo mkuu wa taasisi ya umoja wa miji na serikali za mitaa barani Afrika (UCLG-A) Elong Mbassi anasema miji ikiboreshwa itasaidia ustawi wa jamii lakini zaidi vijana.

(SAUTI MBASSI)

‘Watu wengi Afrika wanaishi katika makazi duni, wengi katika makazi hayo hawana shule,maji safi na huduma za kujisafi na zaidi ya yote hawana ajira. Unatarajia vijana watafanya nini? Kwaiyo lazima sera zetu ziwe sawia.’’

Naye Mkurugenzi wa Mipango wa UN-Habitat Lioune Badiane amesema visa vya ugaidi na vikundi kama Boko Haram na Al Shabab; mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wangozi ni tishio kubwa kwa miji ya Afrika.