Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano kuhusu teknolojia ya angani na udhibiti wa viumbe pori laanza Nairobi

Kongamano kuhusu teknolojia ya angani na udhibiti wa viumbe pori laanza Nairobi

Zaidi ya watu 250 wanaohusika na bayoanuai na udhibiti wa viumbe pori wanakutana jijini Nairobi Kenya kuanzia leo Juni 27 hadi Juni 30, kujadili jinsi teknolojia ya angani inavyoweza kutumiwa katika kulinda viumbe pori na bayoanuai. Taarifa kamili na Joshua Mmali

Taarifa ya Joshua

Kongamano hilo limeandaliwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya Anga za Juu (UNOOSA) kwa ushirikiano na serikali ya Kenya.

Taarifa iliyotolewa na UNOOSA imesema kuwa bayoanuai na viumbe pori vinakabiliwa na hatari kutokana na shinikizo la mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa mazingira na uhalifu wa viumbe pori kote duniani.

Kongamano hilo la Nairobi litaangalia jinsi teknolojia ya angani inavyoweza kutumiwa katika kufuatilia, kutathmini na kudhibiti bayoanuai na mazingira, kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za maendeleo endelevu na mazingira endelevu.