Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utesaji unaendelea kuenea licha ya kupigwa marufuku: Ban

Utesaji unaendelea kuenea licha ya kupigwa marufuku: Ban

Vitendo vya  utesaji  ambavyo ni kinyume na utu vinaendelea kuenea na inasikitisha kwamba vinaendelea kukubalika amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Ameyasema hayo katika tamko lake la kuadhimisha siku ya kimataifa ya usaidizi kwa wahanga wa uteswaji inayoadhimisha kila Juni 26.

Kwa mujibu wa sheria za kimataifa utesaji ni marufuku.

Ban amesema sheria dhidi ya utesaji iko wazi na kuongeza kuwa vitendo hivyo haivafai kutumiwa wakati wowote na katika hali zozote ikiwamo wakati wa machafuko au usalama wa taifa unapokuwa katika kitisho.

Katibu Mkuu amezitaka nchi 159 ambazo zimeridhia mkataba wa kupinga utesaji kusaidia mfuko wa Umoja wa Mataifa wa kupinga utesaji ambao umeanzishwa na baraza kuu la UM mwaka 1981 ukitaka angalau kiasi cha dola milioni 12 kwa mwaka kwa kujitolea.

Mfuko huo husaidia mamia ya mashirika yanayotoa msaada wa kisheria, kijamii, kisaikolojia na kitabibu kwa takribani watu 50,000 kila mwaka wanaokumbana na uteswaji.