Kutojua viwango vya uchafuzi wa hali ya hewa ni changamoto:Prof.Muthama

24 Juni 2016

Kutojua kiwango cha uchafuzi wa hali ya hewa ni changamoto kubwa katika kuhakikisha kwamba mikakati sahihi imewekwa kwa ajili ya kulinda hali hii.

Hiyo ni kauli ya Profesa John Muthama kutoka chuo kikuu cha Nairobi mmoja wa waandishi wa ripoti ya Shirika la Umoja wa Matiafa la mpango wa mazingira, UNEP kuhusu uchafuzi wa hali ya hewa barani Afrika.

Katika mahojiano maalum na Idhaa hii Prof. Muthama amesema kwamba kutojua kiwango cha uchafuzi katika miji mikuu ndio tofauti kubwa kati ya nchi zilizoendelea na zile zinazoendelea hususan zilizo barani Afrika.

Kulingana na ripoti viwango duni vya mafuta ya gari ni changamoto pia kwa bara Afrika Prof. Muthama amesema uchafuzi mwingine mkubwa ni

(Sauti ya Muthama)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter