Skip to main content

Upimaji wa kiwango cha uchafuzi wa hewa ni muhimu katika kuzuia madhara- Muthama

Upimaji wa kiwango cha uchafuzi wa hewa ni muhimu katika kuzuia madhara- Muthama

Takriban watu bilioni tatu wanatumia mafuta yanayochafua mazingira lakini, Ushelisheli waliweza kuimarisha ubora wa hewa ndani ya makazi kwa kubadilisha matumizi ya majiko ya mkaa hadi majiko yaliyo rafiki kwa mazingira.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira, UNEP ambayo inataja hewa chafu kama muuaji wa kimya kimya. Aidha ripoti inasema kwamba nchi nyingi katika bara la Afrika hazijaweka viwango vya ubora wa hewa huku madhara yake yakitajwa kama mauaji ya wengi.

Kufuatia kutolewa kwa ripori hiyo Grace Kaneiya wa Idhaa hii amezungumza na Prof. John Muthama kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, ambaye alishiriki katika ripoti ya ubora wa hewa barani Afrika. Hapa anaanza kwa kuelezea changamoto kuhusu uchafuzi wa hewa.