Ban awaenzi wahanga wa mashambulizi ya Brussels kwenye uwanja wa ndege

15 Juni 2016

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, leo ameweka shahada la maua kwenye uwanja wa ndege jijini Brusses, kukumbuka shambulizi la kigaidi mjini humo mnamo Machi 22, 2016, ambapo watu 32 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa.

Miongoni mwa walioshuhudia hafla hiyo ni maafisa waandamizi wa Ubegiji na watu waliowasili kwanza kwenye maeneo ya mashambulizi hayo.

Mara tu baada ya shambulizi hilo la mwezi Machi, Ban alitangaza kuwa alikuwa na imani kuwa dhamira ya Ubelgiji na Ulaya ya kulinda haki za binadamu, demokrasia na kuishi kwa amani, itaendelea kuwa njia bora na ya kudumu, katika kujibu chuki na ukatili huo.

Katibu Mkuu amesema shambulizi hilo halikuwa tu dhidi ya Ubelgiji, bali lilikuwa dhidi ya ubinadamu wote, kwani mashambulizi yaliyofanyika uwanja wa ndege na kituo cha treni, yalilenga mahali wanapokutana watu kutoka nchi mbalimbali.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter