Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za kutokomeza Ukimwi duniani #HLM2016AIDS

Juhudi za kutokomeza Ukimwi duniani #HLM2016AIDS

Mkutano wa ngazi ya juu wa siku tatu wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu namna ya kukomesha maambukizi ya Ukimwi umfungwa Ijumaa mjini New York.

Huu ni mkutano uliowaleta pamoja, mawaziri wa afya kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, asasi za kiraia, wanaharakati wa makabiliano dhidi ya Ukimwi, mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wengine.

Mjadala umejikita  katika umuhimu wa kuongeza juhudi za vita dhidi ya ukimwi kwa miaka mitano ijayo ili kuiweka dunia katika msitari wa kutokomeza kabisa maradhi hayo ifikapo mwaka 2030 katika sehemu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDG's.