Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ould na Zerrougui wakaribisha tangazo la kuachiwa huru watoto wafungwa Yemen

Ould na Zerrougui wakaribisha tangazo la kuachiwa huru watoto wafungwa Yemen

Wajumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wamekaribisha makubaliano ya pande kinzani kwenye mzozo nchini Yemen ya kuwaachia huru watoto wote wafungwa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani hii leo, msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amewataja wajumbe hao maalum kuwa ni Ismail Ould Cheikh Ahmed wa Yemen na Leila Zerrougui anayehusika na watoto walio kwenye mizozo.

Bwana Dujarric amenukuu wajumbe hao wakisema..

(Sauti ya Dujarric)

“Kitendo cha kuachia watoto hao huru bila masharti yoyote kilikubaliwa na pande zote na kwamba utaratibu wa kuwaachia huru wafungwa unapaswa kushughulikiwa.”