Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lajadili ushirikiano wa UM na AU kuhusu amani usalama

Baraza la Usalama lajadili ushirikiano wa UM na AU kuhusu amani usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekuwa na mjadala wa wazi kuhusu ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika (AU) katika masuala ya amani na usalama. Taarifa kamili na Assumpta Massoi

(Taarifa ya Assumpta)

Mjadala huo wa wazi umehudhuriwa na kuhutubiwa na Mkuu wa idara ya operesheni za ulinzi wa amani katika Umoja wa Mataifa, Herves Ladsous, Kamishna wa amani na usalama katika AU, Smail Chergui, na mwenyekiti wa Kamisheni ya ujenzi wa amani katika Umoja wa Mataifa, Balozi Macharia Kamau.

Katika hotuba yake, Bwana Herves Ladsous amesema kuwa ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na AU katika masuala ya amani na usalama umekuwa ukiimarika, akitaja baadhi ya hatua za ufanisi zilizotokana na ushirikiano huo katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Somalia.

Aidha, amesema ushirikiano huo ni muhimu sana, hasa kwa kuzingatia kuwa asilimia 80 ya shughuli za ulinzi wa amani zinaendeshwa katika bara la Afrika.

Sauti ya Ladsous

“Asilimia 50 ya walinda amani wote wanatoka nchi wanachama wa AU. Kwa hiyo, hii pekee inatosha kuonyesha haja ya ubia imara, ili kujaribu kumaliza migogoro na kuunga mkono juhudi za amani.”