Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya iheshimu haki na uhuru wa kukusanyika:UM

Kenya iheshimu haki na uhuru wa kukusanyika:UM

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa imesema inatiwa wasiwasi na ongezeko la ghasia kufuatia wiki nzima ya maandamano nchini Kenya. Kwa mujibu wa ofisi hiyo jana watu watatu wameripotiwa kuuawa , wawili wakipigwa risasi na polisi mjini Siaya Magharibbi mwa Kenya karibu na mpaka na Uganda huku mmoja akidaiwa kuuawa na polisi mjini Kisumu.

Watu wengine wengi wakiwemo polisi wamearifiwa kujeruhiwa . Maandamano yamezuka pia katika miji mingine ikiwemo mji mkuu Nairobi. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.

(SAUTI YA COLVILLE)

“Tunaitaka serikali kuhakikisha vitendo hivi vya ghasia havirudii na kuheshimu haki ya kukusanyika kwa amani. Pia tunatoa wito kwa waandamanaji kuandamana kwa amani na kutojihusisha na ghasia kama ambavyo imejitokeza wiki iliyopita na katika maanadamano ya wiki hii.”

Ofisi ya haki za binadamu imeongeza kuwa picha na video zikionyesha polisi wabnavyo wapiga na kuwaadhibu waandamanaji inazua maswali endapo vikoso vya usalama Kenya vinazingatia sheria za kimataifa dhidi ya matumizi ya nguvu kupita kiasi.