Skip to main content

Wanawake wanapata matumaini kuona walinda amani wanawake

Wanawake wanapata matumaini kuona walinda amani wanawake

Uwepo wa askari na polisi wanawake kwenye operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa umesaidia harakati za chombo hicho kuhakikisha haki za wanawake na watoto wa kike zinalindwa.

Private Bimkubwa Mohammed, mlinda amani kutoka Tanzania anayehudumu katika kikosi cha mapigano FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC amesema hayo akihojiwa na idhaa hii kuelekea siku ya walinda amani duniani.

(Sauti ya Bimkubwa)

Private Bimkubwa ambaye kituo chake cha kazi sasa ni Beni, Kivu Kaskazini akaelezea hata hivyo changamoto anazokumbana nazo

(Sauti Bimkubwa)

Mahojiano kwa kina na Private Bimkubwa yatapatikana kwenye tovuti yetu.