Skip to main content

Kuelekea mkutano wa masuala ya kibinadamu, ukanda wa Pacifiki kunufaika

Kuelekea mkutano wa masuala ya kibinadamu, ukanda wa Pacifiki kunufaika

Nchi kadhaa kutoka mataifa ya Pacifiki zimethibitisha ushiriki wao katika mkutano kuhusu masuala ya kibinadamu mjini Istanbul Uturuki ( WHS) unaoanza mnamo mwezi Mei 23.

Taarifa ya tovuti ya mkutano huo, WHS inasema kuwa wadau takribani 200 kutoka ukanda huo wanatarajiwa kuhudhuria na kubadilishana uzoefu katika kukabiliana na majanga na mabadiliko ya tabianchi katika mijadala mikuu.

Nchi 15 zimethibitisha kutuma maafisa wa ngazi za juu zikiwamo Fiji, Tuvalu, the Cook Islands, Nauru na Vanuatu.

Kiasi cha wadau 6000 wanatarajiwa kukutana katika mkutano huo kuhusu masuala ya kibinadamu ambao unaelezwa kuwa ni fursa ya kipekee kwa ukanda wa Pacifiki kurekebisha mfumo wa kibinadamu.