Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia zafurusha maelfu CAR

Ghasia zafurusha maelfu CAR

Zaidi ya watu 10,000 wamekimbia makwao kwenye maeneo ya kaskazini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR kutokana na ghasia zilizoibuka wiki hii.

Kwenye taarifa yake Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu OCHA imeeleza kwamba mashambulizi baina ya vikundi vya waasi yamelenga pia raia ambao wengi wamekimbia kwenye miji jirani na kutafuta hifadhi kwa ndugu.

Juu ya hayo OCHA imesema kwamba dhoruba kali imeleta uharibu mkubwa kwenye mji wa Koui ambapo wakimbizi wa ndani kadhaa walikuwa wametatufa hifadhi.

Aidha OCHA imesema mpango kazi wa kuleta usadizi wa kibinadamu wa dharura unajadiliwa hivi sasa.