Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola milioni 360 zahitajika kukabili athari za ukame Zimbabwe:OCHA

Dola milioni 360 zahitajika kukabili athari za ukame Zimbabwe:OCHA

Shirika la Umoja wa mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA, limesema mashirika takribani 45 ya kibinadamu nchini Zimbabwe yanasaka dola milioni 360 ili kutoa msaada wa kuokoa maisha kama chakula, afya, maji na usafi na vifaa vingine vya kujilinda kwa watu milioni 1.8.

OCHA inasema ukame mkali uliochangiwa na El Niño umeongeza njaa na hali ngumu ya maisha kwa watu wasiojiweza nchini Zimbabwe na kuwaacha watu karibu milioni tatu ikiwa sawa na asilimia 21 ya watu wote nchini humo wakiwa hawana uhakika wa chakula.

Shirika hilo limesema waathirika mbali ya binadamui pia mifugo mingi inakosa maji na chakula na kufa.