Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku za kufaidika na uhalifu kutoka kwa wanyama pori zimekwisha:CITES

Siku za kufaidika na uhalifu kutoka kwa wanyama pori zimekwisha:CITES

Ongezeko la uhalifu wa wanyamapori limekutana na juhudi kubwa za jumuiya ya kimataifa za kupambana nao, amesema mtaalam wa Umoja wa Mataifa Jumatatu.

John Scanlon, ambaye ni mkuu wa mkataba wa biashara ya kimataifa dhidi ya viumbe vilivyo katika hatari ya kutoweka CITES , amesema makubaliano ya kimataifa ambayo yanasimamia biashaya ya wanayama pori yanasema kwamba magene ya kimataifa ya wahalifu sasa yanafanya kazi katika kiwango cha viwanda vidogo.

Lakini amesema ana matumaini kwamba mkutano ujao wa kimataifa kuhusu wanyama pori utakaofanyika Johannesburg utasaidia kujipenyeza katika shughuli hizo haramu na kukabiliana nazo.

(SAUTI YA JOHN SCANLON)

"Siku za uhalifu wa wanyamapori kuwa na faida kubwa na hatari ndogo zimekwisha, na katika mkutano wa Johannesburg wa Septemba mwaka huu tumevunja rekodi ya kuwa na agenda yenye vipengele 175, hatujawahi kuwa na agenda kubwa kama hii katika miaka 42 ya kongamano hili. Wadau walisimama wima Bankgong mwaka 2013 na kuweka misimamo mikali pamoja na kuchukua hatua na mwaka huu wa 2016  watajizatiti na kukaza zaidi misumari"