Skip to main content

Hatua madhubuti na za pamoja zitahitajika kutimiza SDGs- Ban

Hatua madhubuti na za pamoja zitahitajika kutimiza SDGs- Ban

Hatua madhubuti na za pamoja kwenye kila ngazi zitahitajika katika kutekeleza ajenda ya malengo ya maendeleo endelevu, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Ban amesema hayo wakati wa kikao 2016 cha Baraza la masuala ya Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa kuhusu ushirikiano, likiwa na kauli mbiu: utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu kupitia sera, uvumbuzi na ushirikishaji.

Katibu Mkuu amesema kikao hicho ni ukumbusho wa haja ya kuwa wabunifu katika kuunganisha maeneo matatu ya maendeleo endelevu, SDGs.

“Ni lazima tuhakikishe kuwa hatua kwa kila ngazi ni madhubuti na za pamoja. Katika kufanya hivyo, tunapaswa kushirikiana na wadau wote kuelekea nia ya pamoja ya kusaidia nchi wanachama. Malengo ya SDGs yanaweza tu kutimizwa kwa kukubaliwa kitaifa na mikakati ya mashinani.”