Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa waomboleza kifo cha Papa Wemba

Umoja wa Mataifa waomboleza kifo cha Papa Wemba

Wakati ulimwengu wa muziki ukiendelea kuomboleza kifo cha nguli wa muziki wa rumba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Jules Shungu Wembadio maarufu kama Papa Wemba, Umoja  wa Mataifa nao umeelezea machungu yake kufuatia msiba huo. Joseph Msami na ripoti kamili.

(Taarifa ya Msami)

Nats..

Mwendazake Papa Wemba, na kibao hicho Rail On…enzi za uhai wake!

Nats..

Sasa hatunaye tena…alifariki dunia tarehe 24 jukwaani akitumbuiza kwenye tamasha la muziki huko Abidjan, Cote d’Ivoire.

Umoja wa Mataifa unaomboleza, gwiji huyu wa muziki ambaye pia aliwahi kuwa balozi mwema wa kutokomeza mabomu ya kutega ardhini nchini mwake, DRCongo. Maman Sidikou, mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa DRC amesema Papa Wemba alinyanyua na kueneza utamaduni wa DRC na wa Afrika ulimwenguni kote.

Na kwa mantiki hiyo kazi zake za muziki zitasalia na kumbukumbu kwa kizazi cha sasa na vijavyo.

Sidikou ambaye pia ni Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa DRC, MONUSCO ametuma salamu za  rambirambi kwa serikali ya DRC na familia ya marehemu Papa Wemba.

Nats..