Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msichana aliyekombolewa kutoka Boko Haram aeleza machungu

Msichana aliyekombolewa kutoka Boko Haram aeleza machungu

Nchini Nigeria takribani wanawake na wasichana 2000 wametekwa nyara na kikundi cha kigaidi cha Boko Haram tangu mwaka 2012.Miongoni mwao ni Khadija ambaye akiwa na umri wa miaka 17 alitekwa nyara na kulazimishwa kuolewa na magaidi hao wa Boko Haram. Je ni madhila yapi alipitia akiwa huko utumwani? Na hadi sasa nini kinamtia machungu kila uchao? Assumpta Massoi anakusimulia katika makala hii iliyowezeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.