Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Itikadi kali na ugaidi vinashamiri wakati haki za binadamu zinakiukwa:UM

Itikadi kali na ugaidi vinashamiri wakati haki za binadamu zinakiukwa:UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon na mwakilishi maalumu wa muungano wa Ustaarabu Nassir Abdelaziz Al-Nasser,wametoa witi wa kushughulikia mizizi ya vikundi vyenye itikadi kali.

Wito huo umetolewa Jumanne wakati wa unzinduzi wa kongamano la 7 la kimataifa muungano wa ustaarabu mjini Baku Arzabeijan chini ya kuali mbiu “kuishi pamoja katika jamii jumuishi ni changamoto na leo letu

Katika ujumbe wake kwa njia ya video Ban amesema Umoja wa mataifa unashirikiana na dunia kutatua migogoro, kuleta Amani na kujikita katika kuzuia chanzo cha migogoro hiyo..

(SAUTI YA BAN)

“Suala hili la itikati kali, chanzo chake sio kwenye dini moja, eneo, taifa au kundi la kikabila. Kuwasonta vidole watu ni hatari na kunavuruga utulivu. Kutia chumvi kunaweza kuuza magazeti lakini hakutatui matatizo”

Naye Nassir Abdelaziz Al-Nasser, akichangia katika hilo amesema maendeleo endelevu hayawezi kupatikana bila amani na usalama, na wakati huo huo amani na usalama vitakuwa hatarini bila maendeleo endelevu.