Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chanjo ya homa ya manjano ni muhimu kwa waendao Angola:WHO

Chanjo ya homa ya manjano ni muhimu kwa waendao Angola:WHO

Wakati juhudi za kudhibiti kuenea kwa homa ya manjano zikiendelea nchini Angola, shirika la afya duniani WHO linawakumbusha wasafiri wote waendao nchini humo kwamba wanahitaji kupata chanjo ya homa ya manjano ili kuthibitisha wamejikinga na kuzuia kuisambaza zaidi. Amina Hassan na ripoti kamili.

(Taarifa ya Amina)

Akizungumzia homa hiyo ya manjano, Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Margaret Chan amesema mlipuko huo nchini Angola unahusishwa na kubainika  pia kwa ugonjwa huo katika nchi zingine za Afrika na Asia, na WHO inahofia hasa maeneo ya mijini kuwa yako hatarini. Hivyo amesisitiza kila mtu ni lazima achanjwe kabla hajasafiri  na kubeba kadi yake. Tarik Jašarević ni msemaji wa WHO

(SAUTI YA TARIK)

“Tangu kuzuka kwa ugonjwa huo Angola mwezi Desemba 2015 kunashukiwa kuwepo visa Elfu Moja mia Tisa Sabini na TAno,  na kati yao 258 wamepoteza maisha, na wengi wao kutoka mji mkuu  Luanda na majimbo mengine mawili Tizawambo na Benguela"