Kamati ya haki za wafanyakazi wahamiaji yahitimisha kikao cha 24

Kamati ya haki za wafanyakazi wahamiaji yahitimisha kikao cha 24

Kamati ya kulinda haki za wafanyakazi wahamaiaji na familia zao imehitimisha kikao chake cha 24 leo jijini Geneva Uswisi, baada ya kuridhia maoni na mapendekezo kuhusu ripoti za Mauritania, Lesotho, Senegal na Uturuki.

Mapendekezo hayo ya hitimisho yatachapishwa kwenye tovuti ya kikao hicho mnamo Jumatatu Aprili 25 2016, mchana.

Aidha, Kamati hiyo imeridhia mapendekezo mawili ya ushirikiano na taasisi za kitaifa na kuhusu mkasa wa hivi karibuni kwenye Bahari Mediterenia.

Wakati wa kikao hicho, Kamati hiyo ilikutana na wawakilishi wa Shirika la Kuhudumia Watoto (UNICEF) wakati ikizingatia suala la watoto katika muktadha wa uhamiaji, na kupata thibitisho la ufadhili kwa mtalaam atakayetoa maelezo zaidi kuhusu suala hilo.