Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msichana kutoka Tanzania awakilisha vijana unapotiwa saini Mkataba wa Paris

Msichana kutoka Tanzania awakilisha vijana unapotiwa saini Mkataba wa Paris

Mkataba wa Paris kuhusu tabianchi unaanza kutiwa saini katika hafla maalum kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani kuanzia leo asubuhi, tarehe 22 Aprili 2016.

Kuanza kutwia saini mkataba huo uliopitishwa mwezi Disemba mwaka jana huko Paris, Ufaransa, ni ishara kuu ya dhamira ya viongozi wa dunia kuanza kuutekeleza kwa kuchukua hatua zitakazobadili mwelekeo wa mabadiliko ya tabianchi, na kuhakikisha viwango vya ongezeko la joto duniani vinasalia chini ya nyuzi joto mbili.

Wawakilishi wa mataifa 160 wanatarajiwa kushika kalamu zilizoandaliwa mahsusi kwa utiaji saini Mkataba huo utakapofunuliwa, na utasalia wazi kwa ajili ya kutiwa saini hadi tarehe 22 Aprili mwaka 2017.

Atakayefungua hotuba za siku hii ya kihistoria ni mwakilishi wa vijana, Gertrude Clement, msichana mwenye umri wa miaka 16 kutoka Mwanza, Tanzania, na mwanahabari mtoto kutoka mtandao wa wanahabari watoto wa Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF.

Katika mahojiano na idhaa hii, Gertrude anaeleza kilichochangia yeye kuwa ndiye anayewakilisha vijana

(Sauti ya Gertrude Clement)

Gertrude ametueleza pia kuhusu jinsi anavyohisi.

(Sauti ya Gertrude Clement)