Ukame waikumba Haiti, WFP yatoa wito

Ukame waikumba Haiti, WFP yatoa wito

El-Nino, mchakato wa hali ya hewa uliofuatia kuongezeka kwa halijoto ya bahari ya Pacifiki, hivi sasa umeenea karibu duniani kote na kusababisha aidha mafuriko ama ukame  na nchini Haiti umeleta ukame.

Ukosefu wa mvua umesababisha upungufu wa asilimia 82 ya mavuno na mfumuko wa bei za vyakula wa asilimia 60.

Hali hiyo imesababisha Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula kuchukua hatua. Kulikoni? Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.