Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka mmoja baada ya tetemeko la Nepal, WFP yajikika katika ujenzi mpya:

Mwaka mmoja baada ya tetemeko la Nepal, WFP yajikika katika ujenzi mpya:

Mwaka mmoja baada ya tetemeko kubwa la ardhi lililouwa watu zaidi ya 9,000 na kusababisha uharibifu wa hasara ya dola takribani bilioni 7 nchini Nepal, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP linashirikiana na serikali ya nchi hiyo ili kuhakikisha wale walio na shida ya chakula wasiachwe nyuma.

Watu walioathirika zaidi na tetemeko hilo , ndio waliopoteza kila kitu amesema Pippa Bradford, mwakilishi na mkurugenzi wa WFP nchini Nepal. Amesisitiza kwamba kuhakikisha msaada unawafikia walengwa ni muhimu sana ili asisahaulike hata mmoja na kusalia nyuma.

WFP ilitoa msaada wa chakula kwa watu milioni 2 katika wiki sita za kwanza baada ya tetemeko, na imekuwa ikitumia msaada wa chakula kuwasaidia ujeni mpya kwa kuwapa watu fedha taslimu au chakula ili wajenge upya miundombinu ya jamii zao.

Mwaka jana mfumo wa umwagiliaji ulioharibiwa na tetemeko hilo ulikarabatiwa pamoja na baadhi ya barabara zilizobomoka.