Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika tunayotaka inaomba utashi wa viongozi: Eliasson

Afrika tunayotaka inaomba utashi wa viongozi: Eliasson

Leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani kunafanyika kongamano Ia ngazi ya juu kuhusu ajenda ya maendeleo ya bara la Afrika, itwayo “Afrika tunayotaka”.

Lengo la mkutano huo ni kuangazia jinsi ya kuhakikisha utekelezaji wa ajenda ya maendeleo ya Afrika ifikapo mwaka 2063, sambamba na ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030.

image
Barabara mjini Addis Ababa. Picha kutoka video ya UNIFEED.
Maeneo yanayopewa kipaumbele na kongamano hili ni uwezeshaji wa wanawake, ukuaji jumuishi wa kiuchumi, ushirikiano wa kikanda na usalama bora.

Akihutubia uzinduzi wa kongamano hilo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson amesisitiza umuhimu wa kushirikisha zaidi wanawake, kuzuia mizozo ili kukuza amani na maendeleo na hatimaye kuimarisha ufadhili wa maendeleo kupitia ushuru na usaidizi wa kimataifa. Aidha amezingatia

image
Naibu Katibu Mkuu Jan Eliasson. Picha ya UN.
(Sauti ya Jan Eliasson)

“Tunahitaji mshikamano, siyo tu kutoka kwa serikali, lakini pia mabunge, jamii, sekta binafsi tukitaka kutimiza malengo hayo makubwa. Malengo hayo yanahitaji hatua thabiti ili kuridhisha matarajio na matumaini yaliyoibuka duniani kote.”

image
Ruhakana Rugunda, Waziri Mkuu wa Uganda. Picha ya UN/Eskinder Debebe.
Naye Waziri mkuu wa Uganda Ruhakana Rugunda amesema ajenda ya Muungano wa Afrika na ajenda ya mwaka 2030 ni fursa kubwa ya kutokomeza umaskini barani humo, akieleza kwamba tayari jamii na viongozi wamehamasishwa na malengo hayo.
image
Mukhisa Kituyi, Katibu Mkuu wa UNCTAD, Picha ya UN/Jean-Marc Ferre.
Kuhusu ushirikiano wa kimataifa, Katibu Mkuu wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD, Mukhisa Kituyi, amesema ni lazima serikali za kiafrika ziraisishe biashara baina za nchi, hasa kupitia malipo ya kidigitali.

(Sauti ya Bwana Kituyi)

“Nasihi sana Afrika kuangalia jinsi ya kuimarisha mikataba ya biashara huru ndani ya Afrika. Unataka biashara huru zaidi na Afrika, tayari masoko yamehurika mno (you are over liberalized) na Ulaya. Ahadi unazopewa kama motisha kwa mikataba ya biashara huru zinaondolewa kabisa wakati nchi hizi zinaingia kwenye ubia kama ule wa Transpacifik.”

image
Naibu Mwenyekiti wa Kamisheni ya Muungano wa Afrika Erastus J.O Mwencha. Picha ya UN

Kwa upande wake, Naibu Mwenyekiti wa Kamisheni ya Muungano wa Afrika Erastus Mwencha akihojiwa na idhaa hii amesema tayari viongozi wameonyesha utashi wao na sasa…

(sauti ya Mwencha)