Skip to main content

Kwa nini hedhi iwe kikwazo kwa mtoto wa kike kusoma?

Kwa nini hedhi iwe kikwazo kwa mtoto wa kike kusoma?

Lengo namba Nne la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linatoa wito kwa kila mkazi wa dunia bila kujali jinsia au hali ya kiafya ikiwemo mzunguko wa hedhi kwa wasichana.

Kama hiyo haitoshi lengo namba Tano linataka usawa wa kijinsia na kujenga uwezo kwa wasichana na wanawake hviyo basi elimu kwa wasichana barubaru ni msingi wa kufanikisha malengo haya. Je harakati zipi zinafanyika?

Benki ya Dunia inatekeleza miradi mbali mbali ikiwemo hatua ya karibuni ya kupiga chepuo mpango wa #Letgirlslearn unaosongeshwa na Michelle Obama, mke wa Rais wa Marekani kama anavyosimulia Assumpta Massoi kwenye makala hii.