Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo Julai 18 ni siku ya Mandela duniani:aenziwa

Hafla ya upanzi wa mti wa Mandela (Picha/um/Eskinder Debebe/NICA)

Leo Julai 18 ni siku ya Mandela duniani:aenziwa

Kila mwaka, tarehe 18 Julai imekuwa ikiadhimishwa kama Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela, tangu siku hiyo ilipoanzishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo Novemba 2009, ili kuenzi mchango wa Hayati Nelson Mandela kwa kukuza demokrasia, haki kwa watu wa rangi zote na maridhiano.

Mwaka huu, siku hiyo imeadhimiswa kwa mara ya kwanza tangu kifo cha shujaa huyo wa uhuru na haki nchini Afrika Kusini, ambaye aliiaga dunia mnamo tarehe 5 Disemba 2013, akiwa na umri wa miaka 95.