Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jamii ya kimataifa saidieni sitisho la mapigano liendelee Syria- de Mistura

Jamii ya kimataifa saidieni sitisho la mapigano liendelee Syria- de Mistura

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria Staffan de Mistura amefungua tena mazungumzo ya amani kuhusu nchi hiyo huko Geneva, Uswisi akisihi jamii ya kimataifa itie shime ili kuepusha ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano nchini humo.

Amesema hayo alipozungumza na wanahabari baada ya kukutana na wajumbe wa upinzani nchini Syria HNC waliodai kuwa sitisho hilo linakiukwa na mwezi Machi pekee watu 21 wameuawa katika matukio yaliyochochewa na serikali.

De mistura amesema ingawa mwelekeo sasa ni kuchagiza mchakato wa mpito wa kisiasa, ukiukwaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano na kumaliza chuki ni tishio kwa mchakato mzima hivyo..

 “Nadhani itakuwa sahihi, kwa sababu iwapo matukio ya ukiukwaji yatakuwepo mara kwa mara yanaweza kuzorotesha azma na imani kwenye mchakato husika. na ndiyo maana pengine itakuwa wakati mzuri kwa wale ambao wamekuwa wanaunga mkono sitisho la mapigano  kuendelea kufanya hivyo na kulinda. Kwa sababu katika awamu ya pili ya mazugumzo itkakuwa ni msaada mkubwa.”

Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa kwa Syria pia amegusia wasiwasi wake kuhusu hali mbaya ya kibinadamu kwenye baadhi ya maeneo ya Syria huku akisisitiza kusongesha mbele suala la msingi la mpito wa kisiasa.