Hatuhusiki katika makubaliano kati ya EU na Uturuki: UNHCR

Hatuhusiki katika makubaliano kati ya EU na Uturuki: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuudumia wakimbizi UNHCR sio sehemu ya muafaka kati ya Uturuki na Muungano wa Ulaya wa kukabiliana na wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji wanaoingia Ugiriki hatua ambayo imeanza kufanya kazi.

Shirika hilo limesema licha ya kwamba halijahusihwa katika muafaka huo lakini wanafuatilia kwa karibu zoezi hilo kama anavyofafanua msemaji wake Arian Rummery ambaye amezungumza katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa.

( SAUTI ARIAN)

‘‘Tumepokea taarifa za hivi karibuni kuwa watu wamechanganyikiwa sana, katika eneo ambalo zoezi limeanza mapema juma lililopita, watu wanahofia hali zao na nini kitawakuta baadaye.’’

Amesema haki za bindamu zinapaswa kulindwa katika zoezi hilo mathalani ulinzi kwa wakimbizi na wahamiaji hao na akaongeza kuwa wakati huu hali ni tete kutokana na mifumo kuzidiwa uwezo.