Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA kuisaidia Brazil kuhusu usalama wa nyuklia wakati wa Olimpiki:

IAEA kuisaidia Brazil kuhusu usalama wa nyuklia wakati wa Olimpiki:

Shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA na serikali ya Brazil wametia saini makubaliano hii leo yenye lengo la kuimarisha hatua za usalama wa nyuklia kwa ajili ya mashindano ya michezo ya olimpiki na olimpiki ya watu wenye ulemavu itakayofanyika Rio de Janeiro baadaye mwaka huu.

IAEA itaipa Brazil vifaa vya kubaini mionzi ya nyuklia na msaada mwingine wa usalama wa nyuklia kwa ajili ya shughuli za michezo ambayo itaanza Agost 5 hadi 21 na ile ya Agost 7 hadi 18. Pande zote mbili pia zimeafiki kubadilishana taarifa kuhusu usafirishaji haramu na shughuli zingine zinazohusiana na nyuklia na nyenzo za mionzi ambazo hazijaruhusiwa .

Makubaliano hayo yametiwa saini mjini Rio de Janeiro na Renato Machado Cotta, Rais wa kamisheni ta taifa ya nishati ya nyuklia Brazil (CNEN), na Khammar Mrabit, mkurugenzi wa kitengo cha usalama wa nyuklia cha IAEA.

IAEA imeshahusika siku za nyuma kusaidia katika matukio makubwa ya michezo kuhakikisha usalama baadhi ikiwa michezo ya mataifa ya Amerika iliyofanyika Rio de Janeiro in 2007na Guadalajara, Mexico, 2011; pia Olimpiki ya 2008 Beijing na kombe la dunia la 2010 Afrika ya Kusini na Brazil 2014.