Tudhamirie upya kupinga ubaguzi wa rangi na kuenzi urithi wa Afrika- Ban

25 Machi 2016

Ikiwa leo ni siku ya kukumbuka wahanga wa utumwa na biashara ya utumwa ya kuvuka bahari ya Atlantiki, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesihi ari mpya katika kupinga ubaguzi wa rangi na kusherehekea urithi wa bara Afrika, ambao umeendeleza jamii kote duniani.

Ban amesema ni lazima uwepo ushirikiano kupigania usawa wa fursa, haki, na maendeleo endelevu kwa watu wenye asili ya Afrika.

Amesema mchango wa Afrika ni dhahiri katika muziki, Sanaa, vyakula na fasihi, vyote vikiwa vinarutubisha utamaduni wa sasa.

Siku hii hutumiwa kuenzi mamilioni ya Waafrika walioondolewa kwa lazima kutoka kwa familia na ardhi za babu zao kwa kipindi cha mamia ya miaka, na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kumbuka utumwa: kusherehekea urithi wa Waafrika ughaibuni na walikotoka.” 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter