Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban awasili Lebanon kwa ziara ya siku mbili

Ban awasili Lebanon kwa ziara ya siku mbili

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amewasili leo mjini Beirut, Lebanon, kwa ziara ya siku mbili, akiwa ameandamana na Rais wa Benki ya Dunia, Jim Yong Kim, na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Kiislamu, Ahmed Mohamed Ali Al-Madani.

Ujumbe wa Ban unatarajiwa kukutana na Spika wa Bunge, Nabih Berri, Waziri Mkuu, Tammam Salama na Waziri wa Ulinzi, Samir Mokbel na maafisa wengine wa ngazi ya juu.

Aidha, ujumbe wa Katibu Mkuu utatembelea jamii zinazowapa hifadhi wakimbizi wa Syria na Palestina, pamoja na makao makuu ya kikosi cha Umoja wa Mataifa Lebanon, UNIFIL, Naqoura, kusini mwa Lebanon.