Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CSW yafungwa leo, ubakaji waangaziwa

CSW yafungwa leo, ubakaji waangaziwa

Mkutano wa 60 wa kamisheni ya hali ya wanawake CSW unatamatishwa hii leo kwa washiriki wa mkutano  ulioratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN WOMEN kufikia maamuzi ya kusongesha hadhi ya mwanamke duniani kote. Flora Nducha na taarifa kamili.

( TAARIFA YA FLORA)

Miongoni mwa mada zilizojadiliwa kwa takribani majuma mawili ni pamoja na ajenda ya 50-50 ifikapo  mwaka 2030, usawa katika uongozi na maamuzi na ukomeshaji wa ukatikli kwa wanawake ikiwemo  vitendo vya ubakaji vinavyodaiwa kushamiri katika baadhi ya sehemu miongoni mwao Uganda na hasa katika jamii ya watu wa asili ya Karamoja, hatua iliyosukuma washiriki kusikiliza ushuhuda wa hali ilivyo na mbinu za kuukomesha.

Katika mahojiano na idhaa hii baada ya kutoa mada katika mjadala huo, mtawa kutoka kanisa katoliki Uganda Mary Achayo amesema ubakaji umekithiri kutokana na utamaduni wa Karamoja na hivyo.

(SAUTI ACHAYO)