Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wadau wa misaada ya kibinadamu wamezindua kampeni ya kupata fedha kukabili ukame Ethiopia:OCHA

Wadau wa misaada ya kibinadamu wamezindua kampeni ya kupata fedha kukabili ukame Ethiopia:OCHA

Wadau wa misaada ya kibinadamu wamezindua Jumatano klampeni ya siku 90 ya kuchagiza kuhusu haja ya haraka ya kupata fedha kwa ajili ya kukabiliana na mtatizo ya ukame nchini Ethiopia na kushughulikia pengo la misaada ya kibinadamu.Grace Kaneiya na maelezo kamili

(TAARIFA YA GRACE)

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA, Ethiopia hivi sasa inakabiliwa na moja ya majanga makubwa zaidi ya hali ya hewa katika historia kukiwa na watu milioni kumi wanaokabiliwa na kupoteza mavuno na mifugo na kukumbwa na uhaba mkubwa wa maji na hatari ya afya.

Bi, Ahunna Eziakonwa-Onuchie, mratibu wa wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu Ethiopia amesema wamezindua kampeni hii ili kuchagiza kuongezwa kwa fedha za ufadhili kuweza kukabiliana na ukubwa wa tatizo.

Ameongeza kuwa hadi sasa Ethiopia ambayo inahitaji dola bilioni 1.4 kwa ajili ya mwaka 2016, imeshapokea dola milioni 758 tu kutoka kwa serikali na jumuiya ya kimataifa na hivyo bado kuna pengo kubwa sana katika sekta zote.