Skip to main content

Ban alaani mashambulizi ya angani yaloua raia wengi Yemen

Ban alaani mashambulizi ya angani yaloua raia wengi Yemen

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amelaani mashambulizi ya angani yaloelekezwa kwenye soko la al-Khamees katika wilaya ya Mastaba, mkoa wa Hajjah nchini Yemen hapo jana Jumanne.

Taarifa ya Msemaji wa Katibu Mkuu imesema tukio hilo ndilo lililokuwa la kikatili zaidi tangu kuanza mzozo wa Yemen, kwani limeripotiwa kuwaua na kuwajeruhi makumi ya raia, wakiwemo wanawake na watoto.

Mashambulizi hayo ni ya pili yenye ukubwa unaokaribiana katika kipindi cha wiki mbili.

Aidha, taarifa ya msemaji wa Ban pia imesema kuwa Ban amesisitiza haja ya pande zote kinzani kuheshimu wajibu wao chini ya sheria za kimataifa za kibinadamu na haki za binadamu, zikiwemo kanuni za kutofautisha, ukubwa wa nguvu zinazotumiwa na kuchukua tahadhari